Stories
The Explosive’ DJ Exploid …..featured on The Insyder Magazine (Volume 14. No 4 April 2014 Edition >Page 37)
Here Is One Kenyan DJ You All Should Know About…..Read More At|> Ghafla Kenya
Unmasking DJ Exploid..Did You Know This About Him..Read More At|> The Kenyan DAILY POST
DJ Exploid featured on TEN THINGS at Pulse Magazine (Friday Standard Gazette )|Date: 1st Nov/2013
DJ Exploid was signed by Mdundo on” 6th September 2013 ”
and since then he is the only DJ in East Africa whom you can download his short mixes/ringtones via your mobile phone >>Click Here To Download——> Deejay Exploid (Mdundo)
Midundo+ >>>Read More( Taifa Leo Gazette|Date: 4th June/2013 )
DJ wa mashinani apania kupambana na miamba wa mijiniNA PAULINE ONGAJI | On Taifa Leo Gazette|Date: 4th June/2013
KATIKA umri mchanga wa miaka 20 pekee tayari Iddi Mugo Gachoki al-maarufu DJ Exploid, yuko mbioni kuweka alama kwenye fani ya udijei humu nchini.
Mzaliwa wa eneo la Ngurubani, Mwea, katika mkoa wa kati, dijei huyu anafanya kila juhudi kushindana na wenzake kutoka miji mkuu nchini.
Licha ya kuwa anaendelesha shuguli zake katika eneo la mashambani, hajatishikia kushindana na wenzake walio na vifaa na mitambo ya kisasa .
Ni bidii hii ambayo ilimpelekea kutambuliwa kama dijei bora chipukizi katika tuzo za Regional DJ Awards.
DJ Exploid asema alitamani kazii hii akiwa angali katika shule ya msingi na kushika kasi kama mwanafunzi wa shule ya upili.
“Sikusomea katika shule ya bweni hivyo wikendi nilifanya mazoezi ya kazi hii. Nilipomaliza shule mwaka uliopita ndipo nikaamua kufuata ndoto yangu kikamilifu,”
Anasema kutokana na jitihada za kupiga msasa ujuzi wake akiwa mdogo, alipokamilisha masomo ya shule ya upili tayari alikuwa ameanza kupokea mialiko kutokana na kazi yake nzuri.
>> Ni ujuzi huu ambao umemwezesha Dj Exploid kufanikiwa katika nyanja hii.
“Nimepata fursa ya kuburudisha katika sehemu tofauti nchini ikiwa ni pamoja na Jumeira nchini Dubai, Dar-Es Salaam nchini Tanzania, Mombasa, Thika, Embu, Nairobi na Mwea miongoni mwa maeneo mengine,” asema.
Isitoshe, ustadi wake umemwezesha kufanya kazi na baadhi wasanii maarufu kama vile D.N.A, Jua Cali, Jaguar, Mariko, Kenrazy, G-kon, Cartel, Octopizzo, miongoni mwa wengine.
“Kadhalika nimefanya kazi na wasanii wa kimataifa kama vile Fambo, Brain Damage, Tiana na Bugle kutoka Jamaica na Melina Katende wa Amerika.
Hata hivyo asema kuwa bado hajafikia upeo wake kwani anapania kushirikiana na wasanii kama vile Prezzo, STL nakatika ngazi za kimataifa, wanamuziki kama vile Konshens, Chris Martin na Drake.
Alilazimika kujifunza kuhusu fani hii kivyake kwani hangeweza kumudu ada ya juu inayotozwa na vyuo vya kutoa mafunzo haya.
Hilo halikuwa changamoto pekee kwani pia alipata pingamizi kutoka kwa wazazi wake.
“Wazazi wengi huhusisha kazi hii na uhuni. Lakini ni dhana ambayo wazazi wangu walilazimika kubadilisha baada ya muda na badala yake kuanza kuunga mkono uamuzi wangu. Hii ni baada ya kugundua kuwa kazi hii haikuwa inaathiri masomo yangu,” aeleza.
Tofauti na madejei wengine wanaoangazia aina moja ya muziki, Dj Exploid ameamua kwenda hatua zaidi na kujihusisha na aina tofauti za nyimbo,” aeleza.
“Kama dijei, unapaswa kutambua kuwa aina ya wimbo sio muhimu mradi una uwezo wa kuwaburudisha mashabiki kuambatana na umri na hafla,” asema.
Hata hivyo kama wengine katika fani hii, anakubaliana na changamoto za hapa na pale huku tatizo kuu likiwa ni pesa.
Hii hasa ikizingatiwa kuwa sharti ajitambulishe hapa nchini na katika ngazi za kimataifa.
“Tatizo lingine ni ugumu wa kupata mialiko ya burudani. Wakati mwingine nalazimika kusafiri mbali ili kujitafutia mialiko hii,” aeleza.
Hata hivyo asema haja acha tatizo hilo kuzima azima yake ya kuendelea na ndoto yake ya kuwa dijei shupavu kwani amekuwa akiuza sidii mitandaoni ili kupata riziki ya kumsukuma.
Ushauri wake kwa madejei wanaochipuka kama yeye ni kumakinika na kuwa tayari kuwekeza.
“Kama umetambuwa unakipaji, usiache kilale na badala yake kitumie kikamilfu,” asema.
Dj Exploid asema uzuri wa kazi hii ni kuwa inawezesha kukutana na watu mashuhuri halikadhalika kusafiri katika maeneo tafauti nchini,” aeleza.
Mbali na udijei anahusika na masuala ya fashoni, uelekezi wa sinema na kwa sasa anasomea masuala ya video na filamu.
Ndoto yake ni kuwa dijei wa kimataifa na vilevile kipindi chake cha muziki katika stesheni za redio na televisheni hapa nchini, bali na kuwa mmoja wa madijei wanaofahamika nchini. Watch The Video Here|>>
DJ Exploid featured on TAKE TEN at Zuqka Magazine (Friday Nation)|Date: 28th Sept/2012
DJ Exploid featured on TAKE TEN at Zuqka Magazine by Dennis Okeyo (Friday Nation) Date: September 28th/2012